CHARLES BABA AMEHAMIA RASMI MASHUJAA BAND
Bendi ya Mashujaa Band inayomilikwa na MASHUJAA GROUP LTD jana imefanikiwa kumnasa CYPRIAN MBWANA GABRIEL maarufu kama CHARLES BABA kwa mkataba wa miaka miwili.
‘baada ya kupokea ofa nyingi sana kutoka bendi karibu zote maarufu mnazozijua,hatimaye Charles Baba kwa kushauriana na mimi amekubaliana na ofa ya Mashujaa Band,hivyo jana(jumanne tarehe 10 january 2012) Charles amesaini mkataba wa miaka miwili na Mashujaa Band na kwa bahati nzuri alifanikiwa kuutuma mkataba huo jioni na leo hii asubuhi tumeupokea’ amesema Bwana Benard Msekwa leo hii akitoa taarifa rasmi kwa waandishi wa habari
Naye Mkurugenzi wa Mashujaa Band bwana Yohana Gehaz huku akiwa amejawa na furaha alisema ni hatua muhimu kwa bendi amabayo ina miaka miwili sasa katika jitihada zake za kujiendeleza ili kupata mafanikio zaidi katika tasnia ya muziki wa dansi nchini na nje ya nchi
‘kwa upande wa mashujaa band tulipata wazo hili siku ya jumatatu na haraka haraka tukakaa kikao cha dharura za menejimenti na hatimaye tuliamua kuijtosa katisa kuwania sahihi ya Charles baba,ilipofika saa sita tu mchana tukawa tumeshauandaa mkataba na tukapata taarifa kwamba Charles anasafiri ilibidi tumkimbilie airport tukiwa runa mikataba yetu,tulipofika tukakuta ndiyo anaingia kucheck inn ndege,tukajaribu kumshawishi asitishe safari ili aweze kuusoma mkataba na ikibidi ausaini,yeye na meneja wake wakagoma na kwa kutusaidia wakap[okea tu mkataba wakasema watatujibu,hatimaye jana meneja wake kanipigia simu usiku kwamba chrles ameukubali mktaba wetu na ameshausaini’ Yohana akielezea hali ilivyokuwa mbele ya waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa Meneja,bwana Benard Msekwa,Charles Baba anatakiwa kurudi haraka sana ili aweze kuanza kazi haraka kwani mkataba umeanza tarehe 10 mwezi januari 2012.
Mashujaa Band inawatangazia wapenzi wake kwamba Charles Baba atakuwa na show maalumu ya utambulisho siku ya ijumaa tarehe 13,na itasindikizwa na bendi kadhaa zikiwemo Extra Bongo na Mapacha watatu.Pia kutakuwa na mapokezi makubwa siku ya kesho katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimi Julius nyerere,muda mtajulishwa.

